Home Habari za michezo AZIZ KI ATUMIKA KUNADI MCHEZO WA POLISI TZ NA YANGA…VIINGILIO MECHI YA...

AZIZ KI ATUMIKA KUNADI MCHEZO WA POLISI TZ NA YANGA…VIINGILIO MECHI YA LEO VYAPANDA BEI KISA YEYE…


Wakati homa ya mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga dhidi ya Polisi Tanzania ambao utapigwa kesho ikizidi kupamba moto jijini Arusha kiingilio cha chini katika mchezo huo imetajwa kuwa ni shilingi elfu 10,000.

Mchezo huo ambao unatazamiwa kuwa mkali na wa kusisimua kutokana na ubora wa vikosi vyote hasa baada ya mabadiliko katika nafasi kadhaa kuhakikisha kila mmoja anatimiza malengo katika msimu mpya utapigwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo viingilio VIP A na B itakuwa ni Sh150,00, VVIP ni Sh30,000 na Sh10,000 mzunguko.

Afisa Habari wa Polisi Tanzania, Hassan Juma amesema wameweka kiingilio hicho ili kutoa nafasi kwa kila mdau na shabiki kujitokeza kwa wingi kuja kuona usajili mpya wa vikosi hivyo lakini wakishuudia burudani safi kutoka kwa maafande.

Amewataka mashabiki kujitokeza kukata tiketi hizo mapema na kuepuka usumbufu ambao utajitokeza huku akiongeza kuwa anaamini leo wana Kaskazini wote watafurahia kikosi chao ambacho kitaanza na ushindi dhidi ya Yanga.

“Sasa wewe unataka umuone Aziz Ki kwa pesa kidogo unataka uone maufundi ya kocha wetu Mrundi kwa hela ndogo kesho njoo angalia tunavyoaanza vyema Ligi.” alisema Juma.

Ameongeza kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu lakini kutokana na maandalizi ambayo wamefanya anaamini watatoka na ushindi kwani timu yao ni bora kuliko wapinzani wao na wanataka kuwafunga hili timu zingine wawaogope.

Ameweka wazi kuwa Yanga ni bingwa mtetezi wa ligi hivyo wao hawaidharau kabisa lakini waje wakiwa wamejipanga wakijua wana kuja kupambana na Polisi Tanzania ambao msimu huu imekuja kivingine hivyo mchezo hautokuwa mwepesi hata kidogo lazima wataacha alama tatu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Yanga tawi la CCM Mkoa, Shehe Maulid Hussein amesema kama mashabiki matumaini yao kuelekea katika mchezo huo ni makubwa wanaamini lazima watashinda kutokana na kikosi chao kilivyo hasa baada ya kutoka kumfunga mtani wao Simba kwenye ngao ya Jamii.

SOMA NA HII  YANGA YAJIVUNIA KOMBE LA MAPINDUZI, KUONGOZA LIGI