Home Habari za michezo BAADA YA KIFINYO YANGA WAFUNGUKA HAYA

BAADA YA KIFINYO YANGA WAFUNGUKA HAYA

Afisa Habari wa Yanga SC Ally Kamwe

Msemaji wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amedai kuwa wao walimiliki zaidi mpira lakini wapinzani wao, kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya ligi ya Mabingwa Afrika, CR Belouzdad wakamiliki matokeo.

“Tumemiliki mchezo, wenzetu wakamiliki matokeo, It’s Football..Hongera kwao. Hii imekwisha Kituo kinachofuata ni Benjamin Mkapa Daima mbele Nyuma Mwiko,” amesema Ally Kamwe baada ya Yanga kupata kichapo cha goli 3-0.

Desemba 2, Yanga atakuwa na kibaura kingine dhidi ya Al Ahly ya Misri katika Dimba la Mkapa.

SOMA NA HII  SIMBA WASHAURIWA WAACHANE NA SAIDO