Home Habari za michezo SIMBA WASHAURIWA WAACHANE NA SAIDO

SIMBA WASHAURIWA WAACHANE NA SAIDO

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia East Africa Ardio, Nsajigwa Senior ameushauri uongozi wa Klabu ya Simba kuachana na kiungo mshambuliaji wao, Said Ntibazonkiza na badala yake watafute mchezaji mwingine wa kuziba nafasi yake.

Saido (36) raia wa Burundi ambaye amewahi kuichezea Yanga, alisajiliwa na Simba katikati ya msimu uliopita akitokea Geita Gold na kufanya vizuri msimu huo akiibuka mfungaji bora na mabao 17 lakini msimu huu mpaka sasa mechi 8 ambazo Simba wamecheza ana bao moja pekee licha ya kucheza karibu kila mchezo.

“Mchezaji kama Saido msimu uliopita kwa namba ambazo alikuwa nazo inaonesha alikuwa na work-rate kubwa sana uwanjani, lakini msimu huu ulivyoanza imeonekana alitumia nguvu nyingi sana uwanjani kwa sababu anaonekana amechoka humuoni akifika katika meneo kwa wakati.

“Kwa hiyo sio mbaya kama ukimuondoa Saido kwa sababu yeye anacheza direct lakini sasa hivi energy hiyo hana, hivyo ni bora ukamuweka pembeni kisha ukabaki na chama ambaye licha ya kuwa hana kasi sana lakini ana akili kubwa ya uwanjani,” amesema Nsajigwa.

SOMA NA HII  NYOTA WA HISPANIA ANAYETAJWA KUIBUKIA YANGA AFUNGIKIA DILI LAKE