Home Uncategorized NYOTA WA HISPANIA ANAYETAJWA KUIBUKIA YANGA AFUNGIKIA DILI LAKE

NYOTA WA HISPANIA ANAYETAJWA KUIBUKIA YANGA AFUNGIKIA DILI LAKE

 INAELEZWA kuwa Yanga ipo kwenye mazungumzo na kiungo wa zamani wa Azam FC na CD Tenerife ya Hispania, Farid Mussa ili kukamilisha dili lake la usajili ndani ya kikosi hicho.

Habari zinaeleza kuwa Yanga tayari wameshafanya mazungumzo na Farid Mussa kilichobaki kwa sasa ni kusaini dili jipya ili aibukie ndani ya kikosi hicho msimu ujao.

Nyota huyo ambaye yupo Bongo kwa sasa amesema;”Ni kweli nimekuwa nikitajwa kujiunga na klabu nyingi hapa Bongo hilo lipo wazi hasa kwa nyakati hizi za usajili.

“Ukweli ni kwamba kwa sasa mimi ni mchezaji huru na sehemu ambayo nitakuwa itajulikana hivi karibuni kwani uwezo huwa haujifichi na itakuwa wazi,”.

SOMA NA HII  BEKI MPYA MANCHESTER UNITED AMTAJA ALIYEMPELEKA UNITED