Home Uncategorized RASMI KELVIN YONDANI MALI YA POLISI TANZANIA

RASMI KELVIN YONDANI MALI YA POLISI TANZANIA


 RASMI Kelvin Yondani beki wa kati ni mali ya Polisi Tanzania yenye maskani yake Kilimanjaro baada ya kusaini dili la mwaka mmoja.


Beki huyo mkongwe kwenye ramani ya soka la Tanzania ambapo amecheza kwa mafanikio ndani ya Klabu ya Yanga pamoja na Simba amesaini dili la mwaka mmoja akiwa mchezaji huru.

Yondani aliachana na Yanga msimu wa 2019/20 baada ya kushindwana na mabosi hao kwenye suala la kuongeza mkataba mpya baada ya mkataba wake wa awali kumeguka.

Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Frank Lukwaro amesema kuwa malengo makubwa ya kufanya hivyo ni kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Malale Hamsini.
“Malengo yetu ni kuona kwamba timu inapata matokeo chanya na kufikia malengo ambayo tumejiwekea, bado tunazidi kuboresha kikosi kwa mujibu wa ripoti ya mwalimu,” .

SOMA NA HII  YANGA YAFANYA MAAMUZI MENGINE KUHUSU AJIBU