Home Uncategorized UWANJA WA MKAPA LEO NI VITA YA KIBABE, SIMBA NA MAJIMAJI TAMBO...

UWANJA WA MKAPA LEO NI VITA YA KIBABE, SIMBA NA MAJIMAJI TAMBO ZATAWALA


 VITA kubwa Uwanja wa Mkapa leo ni kati ya mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho Simba ambao wataunguruma dhidi ya Klabu ya Majimaji yenye maskani yake Songea kwenye mchezo wa hatua ya raundi ya tatu.

Mchezo huu utapigwa majira ya saa 1:00 usiku ambapo Simba itaingia uwanjani ikiwa na machungu ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya FC Platinum mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Inakutana na Majimaji ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza ikiwa kundi A na mchezo wake uliopita ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Boma FC.

Mshindi wa mchezo wa leo anatinga hatua ya nne hivyo ni vita ya kutetea ubingwa dhidi ya ile ya kuvua ubingwa ambayo ni nia ya Majimaji FC.

Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck ameliambia Spoti Xtra kuwa wanahitaji Kombe la Shirikisho hivyo njia pekee ni kupata ushindi kwenye kila mechi.

“Tunamalengo ambayo tupo nayo ikiwa ni pamoja na kutwaa kombe la Shirikisho hivyo hatuna chaguo, wapinzani wetu tunawaheshimu ila tunahitaji matokeo,” .

Meneja wa Majimaji, Godfrey Mvula ameliambia Spoti Xtra kuwa wamejipanga kuifunga Simba licha ya kwamba inashiriki mashindano ya kimataifa.

Mbali na mchezo utakaouwakutanisha mabingwa watetezi pia kutakuwa na mchezo kati ya Namungo dhidi ya Green Warriors, Uwanja wa Azam Complex. Mtibwa Sugar v Geita Gold Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Yanga wao hawana presha washatinga hatua ya nne baada ya wapinzani wao Singida United iliyokuwa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza kushushwa kwa madaraja mawili. 

SOMA NA HII  RASMI..TSHISHIMBI NA JUMA ABDUL KUIKOSA SIMBA..!!