Home Uncategorized MBELGIJI WA SIMBA AJIPA MATUMAINI KUPINDUA MEZA KIMATAIFA

MBELGIJI WA SIMBA AJIPA MATUMAINI KUPINDUA MEZA KIMATAIFA


 KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck amefunguka kuwa bado anaimani kubwa kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika katika mchezo wa pili wa michuano hiyo dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe kwa kuwa anaamini kikosi chake.

 

Simba imepoteza mchezo wa kwanza wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kipigo cha bao 1-0 katika mchezo uliopigwa wiki hii kabla ya mchezo wa marudiano ambao utapigwa Januari 6, mwaka huu.


Sven amesema bado wananafasi kubwa ya kufuzu hatua ya makundi licha kupoteza mchezo wa kwanza kwa kuwa watacheza kwenye uwanja wa nyumbani huku akiamini kwenye maandalizi yake.

 

“Nadhani bado nafasi ya kufuzu ipo ikiwa tutaendelea kufanya maandalizi ya nguvu kwa sababu hatukupoteza mchezo wa kwanza kutokana na ubora wa wapinzani bali imetokea kutokana na makosa ambayo tulifanya wenyewe.

 

“Unajua tunachokiangalia kwa sasa ni mchezo wa pili, tunacheza nyumbani, tutakuwa na nguvu kubwa ya kupambana, kikubwa kwa sasa ni kuangalia timu inataka nini kiufundi baada ya kuwaona wapinzani wetu, tunataka matokeo makubwa nyumbani,” amesema Sven.


Simba inahitaji ushindi wa zaidi ya bao moja ikiwa nyumbani na itakuwa na kazi ya kulinda lango lake lisitikiswe ndani ya dakika 90.

SOMA NA HII  NYOTA MPYA SIMBA ATUMA UJUMBE HUU KWA BOCCO NA KAGERE