Home Uncategorized WACHIMBAJI WATANO WAFARIKI BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI GAIRO – VIDEO

WACHIMBAJI WATANO WAFARIKI BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI GAIRO – VIDEO


Wachimbaji watano leo Jumapili Juni 9, 2019 wamefariki baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo ya dhahabu, katika kijiji cha Kirama kata ya Kiogwe wilayani Gairo mkoani Morogoro.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa wachimbaji hao wamefukiwa na kifusi cha mchanga wakati wakichimba madini aina ya dhahabu ambayo yameibuka siku za hivi karibuni katika Kijiji cha Iyogwe wilayani Gairo.

Akizungumza Mwenyekiti wa chama cha wachimba madini Mkoa wa Morogoro, Dk Omary Mzeru amesema wamepata taarifa hizo na sasa wanafuatilia zaidi.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA