Home Uncategorized AZAM FC, SIMBA NA YANGA WAGOMBANISHWA NA MSHAMBULIAJI HUYU WA KAGERA SUGAR

AZAM FC, SIMBA NA YANGA WAGOMBANISHWA NA MSHAMBULIAJI HUYU WA KAGERA SUGAR

Kassim Khamis, mshambuliaji wa Kagera Sugar saini yake inawindwa na uongozi wa Yanga, Azam FC na Simba kutokana na uwezo wake mkubwa akiwa ndani ya uwanja hasa kwa kufanikiwa kumiliki mpira na kuzuia asipokonywe mguuni.

Kassim alimvutia kocha mkuu wa Timu ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ Emanuel Amunike kabla ya kumtema dakika za usiku wakati kikosi kinakwea pipa kwenda Misri.

Akizungumza na Saleh Jembe, Khamis amesema kuwa amekuwa akizungumza na viongozi wa timu tofauti wakihitaji kuipata saini yake.

“Ni timu nyingi nimekuwa nikiwasiliana nazo kwa ajili ya kujadili kuhusu mkataba wangu, wakati ukifika nitataja timu ambayo nitakwenda msimu ujao na  itakwa ni ile yenye manufaa kwangu.

“Najua kwamba ni lazima niwe ndani ya uwanja msimu ujao ila kusaini bila kujua hatma yangu ndani ya kikosi itakuwa ni mbaya hivyo acha nitulie kwa sasa,” amesema.

Kassim jana alikuwa miongoni mwa kikosi kilichocheza dhidi ya Pamba FC na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 hivyo kama atabaki ndani ya Kagera Sugar ataendelea kubaki TPL.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA ATAJA SABABU YA KAKOLANYA KUSUGUA BENCHI