Home Uncategorized MOSES KITANDU WA SIMBA, SASA BADO KIDOGO KUTIMKIA KENYA

MOSES KITANDU WA SIMBA, SASA BADO KIDOGO KUTIMKIA KENYA


STRAIKA wa Simba, Moses Kitandu anayekipiga Coastal Union kwa mkopo yupo mguu nje ndani kutimkia kucheza soka la kulipwa katika timu ya KCB.

Kitandu ambaye KCB walivutiwa na uwezo wake msimu wa mwaka 2017/18 Simba ilipocheza michuano ya SportPesa Cup kwa sasa imeelezwa uongozi wa KCB umerejea tena kuzungumza naye.

Akizungumza na SpotiXtra, Kitandu alisema kuwa kuna mipango mingi ambayo anaifikiria kwa sasa ikiwa ni pamoja na kucheza nje ya nchi.

“Mimi ni mchezaji na ninajua kipaji changu hakifichiki na mpango uliopo kwa sasa ni kucheza nje ya bongo kwa kuwa nimeshatoka Tanga kuna mambo nayafuatilia.

“Siwezi kutaja timu ambayo nakwenda kuitumikia kwani mambo bado hayajakaa sawa nina amini mambo yakikamilika nitataja timu ninayokwenda kuchezea,” alisema Kitandu.

SOMA NA HII  YANGA KUWAKOSA WATATU LEO, MUANGOLA NAYE HATIHATI,POLISI TANZANIA MMOJA