Home Uncategorized LIPULI WAMEAMUA KWELI, SASA WANAKUJA NAMNA HII

LIPULI WAMEAMUA KWELI, SASA WANAKUJA NAMNA HII

UONGOZI wa Lipuli umesema kuwa kwa sasa hesabu zao kubwa ni kusuka kikosi makini kitakachojiuza chenyewe kwa kuwavutia wawekezaji msimu ujao.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Lipuli, Clement Sanga amesema kuwa changamoto ya ukata imewapa taabu sana hivyo kwa sasa wamepata somo litakalowafanya wajipange kisawasawa.

“Ukizungumzia msimu wetu wa 2018/19 hatukuwa njema hasa kwa upande wa fedha, sasa tumejipanga kuona msimu ujao tunakuwa na mfumo bora kwenye uendeshaji na kuwa bora zaidi kwenye suala la uchumi.

“Kila mdau aliyetupa sapoti tunasema shukrani ila kwa msimu wetu mpya tutakuwa tofauti kidogo na nguvu zetu zitakuwa kwenye uwekezaji makini,” amesema Sanga.

SOMA NA HII  TUSIJISAHAULISHE CORONA BADO IPO, KILICHOBAKI TUMALIZE MSIMU HUKU TUKICHUKUA TAHADHARI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here