Home Uncategorized LIPULI IPO FITI KUWAVAA POLISI TANZANIA LEO

LIPULI IPO FITI KUWAVAA POLISI TANZANIA LEO


NZEYIMANA Mailo, Kocha Mkuu wa Lipuli amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania.

Lipuli iliyo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 33 baada ya kucheza mechi 29 inamenyana na Polisi Tanzania iliyo nafasi ya sita na pointi zake 45 baada ya kucheza mechi 29.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mailo amesema kuwa malengo makubwa ni kuona kikosi kinapata matokeo chanya.

“Tupo tayari na malengo yetu ni kuona kwamba tunapata matokeo mazuri, kila kitu kipo sawa ni jambo la kusubiri na kuona mambo yatakuaje,” amesema.

Mchezo huo utapigwa Uwanja wa Ushirika, Moshi majira ya saa 10:00 Jioni. 

SOMA NA HII  JEURI YA YANGA IMEJIFICHA HAPA