Home Uncategorized NANGWANDA SIJAONA LEO KUNA BIASHA MOJA TU PEVU KWA WANAUME 22 KUSAKA...

NANGWANDA SIJAONA LEO KUNA BIASHA MOJA TU PEVU KWA WANAUME 22 KUSAKA POINTI TATU


NANGWANDA Sijaona, leo kutakuwa na biashara moja tu kwa wanaume 22 ndani ya uwanja huo kusaka pointi tatu muhimu.

Ndanda FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Meja Msataafu, Abdul Mingange itamenyana na Biashara United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Francis Baraza.

Wataalamu wote wawili malengo yao ni kusepa na pointi tatu ili kujiwekea ufalme wao ndani ya ligi msimu ujao.

Ndanda FC ambao ni wenyeji wapo nafasi ya 16 kibindoni wana pointi 31 huku Biashara United ikiwa nafasi ya 10 na kibindoni ina pointi 40.


Timu zote mbili zimecheza mechi 29 ambapo makocha wote wametamba kuwa wana imani ya kusepa na pointi tatu muhimu.

SOMA NA HII  SIMBA YAINGIA ANGA ZA MTUPIAJI HUYU WA RWANDA, MKALI WA KUFUNGA NA KUTUPIA PASI ZA MWISHO