Home Simba SC JEMBE JINGINE HILI LA KAZI LAJIFUNGA MIAKA MITATU SIMBA

JEMBE JINGINE HILI LA KAZI LAJIFUNGA MIAKA MITATU SIMBA


IMEELEZWA kuwa Klabu ya Al Ahly Benghazi ya Libya imetangaza kuondoka kwa kiungo Sadio Kanoute mwenye umri wa miaka 24 ndani ya kikosi chao.

Kiungo huyo anatajwa kumalizana na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara ambao ni Simba walioweka kambi kwa sasa nchini Morocco.

Dau ambalo anatajwa kupewa nyota huyo ni zaidi ya milioni 300 kwa ajili ya usajili wake na ni dili la miaka mitati ambayo atasaini.

Ni kiungo mwenye uwezo wa kukaba na kushambulia ikiwa atapewa nafasi na uwezo wake ukajibu ndani ya Simba inayonolewa na Didier Gomes.


Jana alitambulishwa kiungo kutoka Senegal hivyo leo inaweza ikawa zamu ya nyota huyo raia wa Mali.
SOMA NA HII  KISA KOCHA MPYA KUTOKA HISPANIA..RAGE AUNYOOSHEA KIDOLE UONGOZI WA SIMBA..AITAJA YANGA...