Home Habari za michezo DILI LA MSUVA NA YANGA ZIIIIII….MATAJIRI WA AFRIKA KUSINI WAMBEBA JUU KWA...

DILI LA MSUVA NA YANGA ZIIIIII….MATAJIRI WA AFRIKA KUSINI WAMBEBA JUU KWA JUU…

Habari za Michezo leo

SIMON Msuva winga mzawa ambaye yupo na timu ya Tanzania, Taifa Stars, Ivory Coast kwenye Kombe la Mataifa Afrika, (AFCON) amesaini dili la miaka miwili Klabu ya Cape Town City ya Afrika Kusini.

Nyota huyo aliwahi kucheza ndani ya kikosi cha Yanga ambapo alikuwa anatajwa kuwa kwenye hesabu za kurejeshwa hapo kwa mara nyingine tena.

Taarifa zimeeleza kuwa mchezaji huyo amesaini dili la mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo hivyo hatajiunga na Yanga wakati huu mpaka wakati ujao ikiwa watafikia makubaliano mazuri.

Timu ya Taifa ya Tanzania inakibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa pili hatua ya makundi wakiwa kundi F itakuwa dhidi ya Zambia.

Januari 21 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa baada ya ule wa awali Januari 17 kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Morocco ambapo Msuva anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaokuwa kwenye kazi hiyo.

Kwa sasa alikuwa mchezaji huru baada ya kutokuwa na timu kwa kuwa ile aliyokuwa awali ilisitisha mkataba wake.

SOMA NA HII  TETESI....MANZOKI KUONEKANA KWENYE SIKU YA WANANCHI YA YANGA....MIPANGO YOTE NI KIMYA KIMYA NAMNA HII...