Home Habari za michezo HIZI HAPA SABABU ZA KIGOGO WA SERIKALI KUIKIMBIA SINGIDA FG..,FIFA WATAJWA…

HIZI HAPA SABABU ZA KIGOGO WA SERIKALI KUIKIMBIA SINGIDA FG..,FIFA WATAJWA…

Habari za Michezo

WAKATI Rais wa Singida Fountain Gate FC, Japhet Makau akikanusha juu ya kujitoa na kuziondoa hisa zake katika Klabu hiyo, imefahamika kuwa kigogo mkubwa hapa nchini mwenye maamuzi makubwa ya kisiasa ambaye awali alikuwa nyuma ya Singida amejitoa  na kuamua kununua timu ya Ihefu FC kutoka maskani yake Mbeya.

Taarifa za uhakika zilizoifikia  Soka la Bongo kuwa kujiondoa kwa kigogo huyo ni kutokana na madeni ya wachezaji walioingia nao mkataba na kuvunjiwa bila ya utaratibu na timu hiyo kupelekea Shirikisho la Soka Ulimwenguni (Fifa) na kufungiwa kusajili.

Mtoa habari huyo alisema ukiachilia mbali madeni hayo lakini kulitokea sintofahamu kati ya wamiliki hao na kufanya kila mmoja kuchukuwa hisa zake na hatimaye kigogo huyo kuamua kuichukuwa Ihefu FC na kuhamisha baadhi ya wachezaji kutoka Singida Fountain Gate FC.

Mbali na wachezaji lakini pia kuna baadhi ya watendaji waliokuwepo Singida Fountain Gate FC ambao walikuwa chini ya kigogo huyo wamehamia Ihefu FC akiwemo Mkurugenzi wa Ufundi Ramadhani Nsanzwirimo, Mtendaji Mkuu Sikwane Olebila na aliyekuwa kocha msaidizi, Mathias Lule.

Rais wa Singida Fountain Gate FC, Makau alisema timu hiyo haikuwa na mtu zaidi yake na ameamua kufanya biashara ya wachezaili ili kuweza kupata fedha ili kuwez kutatua changamoto zinazowakabili ilikiwemo kulipa fedha wachezaji ambao waliachana nao awali.

Amesema wamefanikiwa kuuza baadhi ya wachezaji ndani na nje ya nchini ili kupata fedha ambazo zitawasaidia kuwalipa baadhi ya wachezaji ambao walivunja nao mkataba na kusababisha kufungiwa kusajili na Shirikisho la Soka Ulimweni (Fifa).

Baadhi ya waliondoka ni Gadiel Michael ambaye ameindoka jana kwenda Afrika Kusini kujiunga na klabu ya Cape Town City, Joash Onyango,Duke Abuja, Elvis Rupiah na Habibu Kyombo kwenda Ihefu na Maddie Kagere kujiunga na Namungo FC.

Hata hivyo, duru zetu za uchunguzi kutoka ndani ya klabu hiyo iliyotamba vyema kwenye kombe la Mapinduzi hivi karibuni, zinadani kuwa madai ya Ndugu Makau hayana  ukweli wowote isipokuwa Kigogo huyo wa Serikali aliamua kuchukua wachezaji waliokuwa anawalipa kwa pesa zake na kuwapeleka Ihefu.

 Bw, Mkau alinukuliwa  akisema kuwa katika siku za hivi karibuni kulitokea sintofahamu na mambo mengi kuhusu timu yetu ikiwemo kuondoka baadhi ya wachezaji huku akidai kuwa waliamua kufanya biashara kwa kuwauza baadhi ya nyota wao na fedha zinazopatikana kwenda kutatua changamoto zetu.

Amesema walikuwa na changamoto kwa wachezaji wao walioachana nao kinyume na utaratibu halu iliyopeleka kwenda Fifa na kufungiwa kusajili na sasa wanatafuta fedha ili kuweza kutatua changamoto hizo.

“Singida Fountain Gate FC kazi yetu ni soka na hatuna sehemu ya kuingizia fedha zaidi ya mpira wa miguu kwa kuuza baadhi ya wachezaji na kuongezea na tulizopata katika vyanzo vingine ili kuweza kutatua changamoto tulizokuwa nazo.

Tukaamua kuuza baadhi ya wachezaji ambao wako katika kiwango bora kuweza kupata fedha hizo , lakini kuuza nyota wetu hao hatuwezi kuathiri timu yetu katika mipango yetu ya ligi kuu na mashindano yaliyopo mbele yetu,” alisema Makau.

Aliongeza kuwa maamuzi hayo yaliwashirikisha benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Thabo Senong kuridhia kuondoka kwa baadhi ya wachezaji hao ili kuweza kupata fedha za kulipa na kufunguliwa kwa dirisha kubwa la usajili.

Kwa mujibu wa taaifa yao iliyitolewa  wakitangaza kikosi chao baada ya baadhi ya wachezaji kuondoka huku saba wakidai kutolewa kwa mkopo na wawili kumaliza mkataba.

Walitaja wachezaji waliosalia ndani ya kikosi hicho kwa sasa ni Beno kakolanya, Ibrahim Parapanda, Benedict Haule, Biemesi Carno, Abdulmajid Mangalo, Hamadi Wazir. Khalid Idd. Yahaya Mbegu. Kelvin Kijri. Nicholas wadada. Bruno Gomes . Yusuph Kagoma. Aziz Andabwile na Laurian Makame

SOMA NA HII  KISA UWEZO..SAKHO MFALME MPYA SIMBA..MWENYEWE ASEMA KAZI BADO...YANGA WAIZIDI UJANJA SIMBA...