Home Uncategorized POLISI TANZANIA YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA LIPULI

POLISI TANZANIA YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA LIPULI


SIXTUS Sabilo, mtupiaji namba moja ndani ya Klabu ya Polisi Tanzania amesema kuwa kazi kubwa waliyonayo ni kuendelea pale walipoishia wakati Ligi Kuu Bara iliposimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona.

Hakukuwa na mechi ya ushindani tangu Machi 17 baada ya Serikali kusimamisha masuala ya michezo mpaka pale yaliporuhusisiwa kuanza kutimua vumbi Juni Mosi, na Juni 13 ligi ilianza ambapo leo Polisi Tanzania iliyo chini ya Kocha Mkuu, Malale Hamsini itamenyana na Lipuli ya Iringa.

Akzungumza na Saleh Jembe, Sabilo amesema kuwa kila mchezaji ana morali kubwa ya kusaka ushindi ili kupata pointi tatu.

“Kwenye mchezo kwetu muhimu pointi tatu, tuna amini kwa namna ambavyo tumejipanga kila kitu kitwenda sawa na tutapata pointi tatu ukizingatia kwamba tunacheza nyumbani mashabiki wajitokeze kwa wingi,” amesema.

Sabilo ametupia mabao saba ndani ya Polisi Tanzania iliyofunga mabao 29.

SOMA NA HII  MAKARATEKA KUPEWA SEMINA YA MAFUNZO RUVUMA