Home Uncategorized KMC YAWEKA KANDO KICHAPO CHA MTIBWA SUGAR, HESABU ZAO KWA MABINGWA WATETEZI

KMC YAWEKA KANDO KICHAPO CHA MTIBWA SUGAR, HESABU ZAO KWA MABINGWA WATETEZI


 UONGOZI wa KMC umesema kuwa haukutarajia kupoteza mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri jambo linalowafanya wayaweke kando matokeo hayo na kuanza kuwapigia hesabu mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba.


Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa walicheza mpira kwa kujituma wachezaji wao na kushindwa kupata matokeo.

“Ukizungumzia mpira ambao tulicheza dhidi ya Mtibwa Sugar ulikuwa ni mzuri, mpira kodi, mpira mapato, mpira ushuru ila bahati mbaya hatukupata pointi tatu.

“Kwa kuwa umeshapita tunaachana na matokeo hayo sasa tunatazama mchezo wetu ujao dhidi ya Simba, niwahakikishie mashabiki kwamba tutafanya vizuri na tutapata matokeo kwenye mchezo wetu ujao,” amesema.


KMC ilifungwa bao 1-0 ikiwa ugenini lililopachikwa na Salum Kihimbwa kwa kichwa akitumia mpira uliochongwa na Kanoni uliomshinda mlinda mlango Juma Kaseja.

SOMA NA HII  CHIRWA NDIO BABA LAO AZAM FC, CIOBA AKERWA NA UBUTU WA SAFU YAKE YA USHAMBULIAJI