Home Habari za michezo MANARA AWATOLEA UVIVU TFF KISA CHAMA, AZIZ KI…. ISHU IKO HIVI

MANARA AWATOLEA UVIVU TFF KISA CHAMA, AZIZ KI…. ISHU IKO HIVI

Habari za Yanga

Msemaji wa Klabu ya Yanga aliyefungiwa na TFF, Haji Manara amewakingia kifua wachezaji wa soka wenye mikataba binafsi na kusema kanuni za Shirikisho la mpira Tanzania (TFF) zimekuja kuwanyonya wachezaji ambao ndiyo wadau namba moja.

Manara ambaye amekuwa akiwapigania wachezaji wa soka nchini ili wapate endorsements za matangazo ili kujiongezea vipato vyao, amesema wachezaji wanapaswa kuwa huru kwa ajili ya kujiingizia vipato.

“Tuna TFF ya ajabu kidogo, si vyema kutumia maneno haya, lakini inashangaza kuona wachezaji wanabanwa katika mikataba yao binafsi.

“Alafu cha kushangaza kikitaka kupitishwa kitu wanasema vilabu vimekubali, sidhani kama kuna klabu inaweza kukubali suala hili, kiukweli hii sio fair” alisema Manara.

Miongoni mwa wachezaji wenye mikataba binafsi ni nyota wa Simba SC Mohamed Hussein Tshabalala’ na Stephen Aziz Kl nyota wa Yanga SC.

SOMA NA HII  ACHANA NA HABARI ZA KUPATA SHAVU MISRI...HUU HAPA UKWELI WA MAMBO SIMBA KUKUBALI HARAKA KUMUACHIA ZORANI...