Home Uncategorized WATUPIAJI BONGO WAMTAJA NYONI KUWA MIONGONI MWA VISIKI KUPITIKA

WATUPIAJI BONGO WAMTAJA NYONI KUWA MIONGONI MWA VISIKI KUPITIKA


WASHAMBULIAJI wazawa wamelia na ugumu wa beki kiraka wa Simba, Erato Nyoni kwa namna anavyokuwa kizuizi kwao kufikia malengo yao ya kucheka na nyavu.
Ditram Nchimbi anayekipiga ndani ya Yanga na Daruesh Saliboko anayekipiga ndani ya Lipuli ni miongoni mwa washambuliaji ambao hupiga hesabu kali kupenya kwenye ngome ya Simba iwapo Nyoni atakuwa kikosini.
Akizungumza na SpotiXtra, Nchimbi mwenye mabao sita na pasi mbili za mabao alisema kuwa miongoni mwa mabeki ambao ni pasua kichwa ndani ya Bongo ni pamoja na Nyoni ambaye muda wote ana hatari akiwa uwanjani.
“Kwangu mimi naona Nyoni ni aina ya mabeki ambao wana vitu vingi uwanjani, kukaba, kufunga na kutengeneza nafasi hivyo akiwa uwanjani huyu jamaa ni lazima mshambuliaji usiende kichwakichwa, anatumia sana akili na kipaji chake,” alisema Nchimbi.
Saliboko mwenye mabao nane ndani ya Lipuli alisema kuwa Nyoni ni kisiki kikiwa uwanjani macho yake ni kwenye mpira muda wote huku akitumia zaidi akili.
Simba imefungwa mabao 15 kwenye ligi kuu na kufunga mabao 63 baada ya kucheza mechi 28 huku Nyoni akifunga bao moja.
SOMA NA HII  BALAA LA MWILI JUMBA NDANI YA UWANJA LIPO HIVI