Home Uncategorized SIMBA KUREJEA BONGO BAADA YA KUCHEZESHWA GWARIDE NA PRISONS

SIMBA KUREJEA BONGO BAADA YA KUCHEZESHWA GWARIDE NA PRISONS

 


BAADA ya mchezo wa jana Oktoba 22 kwa kufungwa bao 1-0 kikosi cha Simba kimeanza safari leo kurejea Dar kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting.


Simba ilifungwa bao hilo kwa kichwa na Samson Mangula dakika ya 49 na kuwafanya mabingwa hao watetezi kuziacha pointi tatu Uwanja wa Nelson Mandela.


Mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting utachezwa Uwanja wa Uhuru, Oktoba 26 saa 10:00 Uwanja wa Uhuru.

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck, amesema kuwa kilichotokea ni sehemu ya mchezo hivyo watatumia makosa waliyoyafanya kufanya vizuri mchezo ujao.

“Kilichotokea mbele ya Prisons ni sehemu ya mchezo, kwa sasa tunaelekeza nguvu zetu kwenye mchezo wetu ujao dhidi ya Ruvu Shooting,” amesema. 


Simba ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 13 baada ya kucheza mechi sita ndani ya ligi, kinara ni Azam FC mwenye pointi 21 baada ya kucheza mechi saba na watani zao wa jadi Yanga wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 16.

SOMA NA HII  SANCHEZ AWAGEUZIA KIBAO MAN UNITED, TETESI KIBAO ZA SOKA DUNIANI HIZI HAPA LEO