Home news MAMBO YAMEANZA KWA MKAPA, SIMBA V YANGA

MAMBO YAMEANZA KWA MKAPA, SIMBA V YANGA


LEO Uwanja wa Mkapa saa 11:00 Jioni kutakuwa na mchezo wa kukata na shoka kati ya Simba v Yanga.

Mchezo wa leo unasubiriwa kwa shauku na wadau ambapo tayari jina la mwamuzi wa kati pamoja na wasimamizi wengine wa mchezo huo ipo wazi.

Ni Ramadhan Kayoko huyu atakuwa mwamuzi wa kati na katika masuala ya Waandishi wa Habari ni Cliford Ndimbo yeye atasimamia masuala hayo.

Kwa sasa mashabiki wameanza kujitokeza Uwanja wa Mkapa ambapo Wizara ya Afya ina kampeni yake ya kuwahimiza Watanzania kuchanjwa kwa hiyari kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.

SOMA NA HII  ISHU YA JEZI MPYA ...SIMBA WAIBUKA NA HOJA HII TENA..WATAJA MUDA NA MAHALI ZITAKAPOPATIKANA...