Home kimataifa MANCHESTER HAIJAKATA TAMAA YA UBINGWA

MANCHESTER HAIJAKATA TAMAA YA UBINGWA

 


SARE ya kufungana bao 1-1 dhidi ya West Brom imemfanya Kocha Mkuu wa Manchester United,  Ole Gunnar Solskjaer kusema kuwa haijawatoa kwenye mbio za kuufukuzia ubingwa.


Ikiwa Uwanja wa The Hawthons ilishuhdua bao la mapema kabisa kutoka kwa Mbaye Diagne dakika ya pili na lilisawazishwa na nyota wao Bruno Fernandes dakika ya 44.


Sare hiyo inaifanya United wafikoshe jumla ya pointi 46,wakiachwa kwa tofauti ya pointi 7 na vinara Manchester City wenye pointi 53 na wana mchezo mmoja mkononi kwa kuwa wamecheza jumla ya mechi 23.


West Brom ipo nafasi ya 19 kwenye msimamo ambapo ni nafasi mbaya kwao ikiwa itadumu hapo inaweza kushuka daraja na kibindoni ina pointi 13 baada ya kucheza jumla ya mechi 24.


Ole amesema:”Bado tuna mechi mkononi na bado tunaweza kufanya jambo. Hatutawaruhusu (City) waweze kutuacha. Tutacheza nao hivi karibuni na hatutaacha pointi tatu kwao kirahisi.

SOMA NA HII  TUCHEL ATAJA SABABU YA KUMPA DILI LUKAKU