Home kimataifa INTER MIAMI INAMPIGIA HESABU ASHLEY YOUNG

INTER MIAMI INAMPIGIA HESABU ASHLEY YOUNG

 

IMERIPOTIWA kuwa Ashley Young mwenye umri wa miaka 35 ambaye anacheza nafasi ya winga pamoja na ulinzi ndani ya kikosi cha Inter Milan yupo Kwenye hesabu za Inter Miami.


Beki huyo ambaye amewahi kucheza pia ndani ya Klabu ya Manchester United ameshinda taji la Serie A akiwa chini ya Kocha Mkuu, Antonio Conte jambo ambalo linaikuza thamani yake.


Kutokana na uwezo wa nyota huyo anatajwa kuiacha timu yake msimu utakapomeguka kwa sababu mkataba wake utakuwa umefika ukingoni.

Inter Miami  inayomilikiwa na nyota wa zamani wa Manchester United,  David Beckham, Marcelo Claure, Jorge Mas ipo tayari kushindana na Watford ili kupata saini ya nyota huyo.

Young aliwahi kucheza ndani ya Watford msimu wa 2003/2007 na alicheza jumla ya mechi 110 kabla ya kujiunga na Aston Villa kwa dau la euro milioni 9.65 msimu wa 2007.

SOMA NA HII  KIPIGO CHA 4-0 KUTOKA BRIGHTON CHAWAINUA MASHABIKI MAN UTD...WIBUKA NA MSIMAMO HUU MKALI KWA WENYE TIMU...