Home Uncategorized YANGA WAOMBWA KUENDELEA KUPATA NAKALA YA JARIDA LAO

YANGA WAOMBWA KUENDELEA KUPATA NAKALA YA JARIDA LAO


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa mashabiki wanapaswa waendelee kujipatia nakala ya jarida la timu yao ili kujifunza mengi zaidi.

Hivi karibuni Yanga ilizindua jarida lao maalumu ambalo lina malengo ya kuwapa habari wanachama wao pamoja na mashabiki.

Ofisa Uhamasishaji na Msemaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa ndani ya jarida hilo kuna mambo mengi ambayo yatakuwa ni faida kwa wanachama pamoja na wapenzi wa klabu hiyo.

“Ni jarida zuri na maalumu kwa ajili ya wanaohitaji kupata taarifa zaidi za Yanga pia ni muhimu kujivunia kilicho bora, bei yake ni sh 5,000  ila ukinunua na jezi yenye chapa ya GSM ile orijino unapewa na jarida bure,” amesema.

SOMA NA HII  YANGA: WACHEZAJI WANAFANYA KAZI WALIYOPEWA, TUKIRUDI TUTAKUWA VIZURI