Home Simba SC GADIEL ANAWEZA KUBAKI SIMBA, AJIBU NI PASUA KICHWA

GADIEL ANAWEZA KUBAKI SIMBA, AJIBU NI PASUA KICHWA


 LICHA ya beki wa kushoto wa Simba Gadiel Michael kutokuwa na nafasi kikosi cha kwanza inaelezwa kuwa yupo kwenye mazungumzo na mabosi hao ili kuongeza kandarasi mpya kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Chini ya Didier Gomes, Gadiel amekuwa na ushkaji mkubwa na benchi huku mshikaji wake Mohamed Hussein, akianza kwenye kikosi cha kwanza katika nafasi yake ambayo anaicheza.

Habari zinaeleza kuwa ni mkataba wa Ibrahim Ajibu ambaye ni kiungo unampasua kichwa Gomes kwa kuwa bado hajamuelewa kiungo huyo mshambuliaji aliyejiunga na timu yake ya zamani akitokea Klabu ya Yanga.

Ajibu amekuwa akisugua benchi pia tofauti na kiungo mwenzake Hassan Dilunga ambaye amekuwa akipata nafasi ya kucheza chini ya Gomes.

“Gadiel bado kuna uwezekano akabaki ndani ya Simba kwa kuwa bado hawajapata beki wa kushoto mzawa, ila Ajibu yule kweli ni pasua kichwa bado Gomes hajamuelewa.

“Ikiwa mazungumzo yatakwenda sawa basi anaweza kusaini dili jipya la kuendelea kuitumikia timu hiyo kwa kuwa bado kipaji chake anacho ila anashindwa kujiamini kwa kuwa hajaanza kikosi cha kwanza katika mechi nyingi,” ilieleza taarifa hiyo.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kuhusu wachezaji wa Simba kusaini madili ya kuendelea kuitumikia timu hiyo aliweka wazi kwamba bado mazungumzo yanaendelea na kila kitu kitakuwa sawa.

“Bado mchakato wa kuendelea kuboresha mikataba ya wachezaji inaendelea na kwa wale ambao Simba itawahitaji hawawezi kuondoka kwenda popote, kokote,”.

Miongoni mwa nyota ambao wamesaini madili ya kuendelea kuitumikia timu hiyo ni pamoja na Mohamed Hussein, John Bocco na Shomari Kapombe. 

SOMA NA HII  SIKU CHACHE BAADA YA KUTUA JKT...DILUNGA AFUNGUKA MAPYA KUHUSU ISHU YAKE NA SIMBA...