Home Azam FC AZAM FC YALIPIGIA HESABU KOMBE LA SIMBA

AZAM FC YALIPIGIA HESABU KOMBE LA SIMBA


 UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa nia yao kubwa ni kutwaa taji la Kombe la Shirikisho ambalo lipo mikononi mwa Simba kwa sasa.

Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina imetinga hatua ya robo fainali baada ya kushinda mabao 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa hatua ya 16 bora uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Vivien Bahati, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa bado wanaamini kwamba wana nafasi ya kuendelea kupata matokeo katika mechi zao zijazo.

“Kupita hatua ya robo fainali ni furaha kwetu na bado tuna amini kwamba tuna kazi ya kufanya kwa ajili ya mechi zetu zijazo na tutafanya vizuri.

“Malengo yetu ni kwamba kwenye mechi zetu zilizobaki tutapata matokeo chanya jambo ambalo litatupa nafasi ya kuweza kulipata taji hili ambalo ni kubwa,” amesema. 

SOMA NA HII  MUDATHIR AVUNJA UKIMYA AZAM...AFUNGUKA KINACHOWAKWAMISHA..WACHEZAJI NA KOCHA WATAJWA..