Home Habari za michezo TETESI ZA USAJILI: IBRAHIM AJIB KUVAA UZI WA NJANO TENA…

TETESI ZA USAJILI: IBRAHIM AJIB KUVAA UZI WA NJANO TENA…

Tetesi za usajili bongo

Tetesi za usajili zinasema kuwa Ibrahi Ajibu anatajwa kumalizana na mabosi wa Singida United.

Nyota huyo atajiunga na timu hiyo akitokea ndani ya Azam FC ambao walitoa shukrani kwake kwa huduma yake baada ya mkataba wake kugota ukingoni.

Tetesi za Usajili bongo zinajua kuwa Mkataba wa Ajibu aliosaini ndani ya Azam FC akitokea Simba ulikuwa na kipengele cha kuogeza mwaka mmoja ikiwa ataonyesha kiwango kikubwa lakini licha ya muda ambao amecheza hapo mambo yalikuwa magumu kwake.

Ni dili la miaka miwili anatajwa kupewa ndani ya Singida Big Stars hivyo ataungana na washkaji zake Said Ndemla, Meddie Kagere,Pascal Wawa ambao aliwahi kucheza nao Simba.

Tayari Singida Big Stars imemtambulisha Kibabage ambaye alikuwa anacheza ndani ya Mtibwa Sugar.

SOMA NA HII  USIKAE KINYONGE....BUTUA MAISHA NA ODDS HIZI ZA KIBABE KUTOKA MERIDIANBET LEO...