Home Habari za michezo HUYU HAPA KIUNGO FUNDI ANAYETUA YANGA SC KIBABE…ANATOKEA AS VITA…

HUYU HAPA KIUNGO FUNDI ANAYETUA YANGA SC KIBABE…ANATOKEA AS VITA…

Tchakei Marouf kujiunga na Yanga SC

TAARIFA kutoka DR Congo zinaeleza kuwa Klabu ya Yanga SC ipo katika mazungumzo na Klabu ya AS Vita kwa ajili ya kumsajili kiungo fundi kutoka ndani ya timu hiyo anayefahamika kwa jina la Marouf Tshekai, 26.

Kiungo huyo fundi mwenye uraia wa Togo ameshinda tuzo ya kiungo bora wa Ligi ya DR Congo kwa misimu miwili mfululizo huku akisifika kwa uwezo wake mkubwa wa kupiga mashuti nje ya boksi.

Taarifa    kutoka katika chanzo cha ndani kutoka DR Congo, zinasema kuwa Yanga SC ipo katika mazungumzo na viongozi wanaomsimamia mchezaji huyo ambaye inasemekana kuwa amegoma kuongeza mkataba ndani ya timu hiyo kutokana na ofa mbalimbali anazozipata kutoka klabu mbalimbali ikiwemo Yanga.

“Yanga SC ni kweli wamekuwa kwenye mazungumzo na viongozi wa mchezaji huyo ni kwa namna gani wanaweza kumpata katika dirisha hili dogo la usajili, Marouf ni moja kati ya wachezaji bora ndani ya ligi ya DR Congo kutokana na kushinda tuzo mbili mfululizo za kiungo bora.

“Viongozi wa mchezaji wanashinikiza mchezaji huyo kutokuongeza mkataba wake ndani ya AS Vita kutokana na ofa nyingi wanazopata viongozi wa mchezaji huyo wanaomsimamia ikiwemo ofa ya Yanga,” kilisema chanzo hicho.

Naye meneja wa AS Vita, Dyba Ilunga alisema kuwa: “Kam ni Yanga SC wanamhitaji mchezaji huyu wanafahamu nini cha kufanya. Yanga SC wanauhusiano mzuri na AS Vita na mara kadhaa wamekuwa na mawasiliano na Rais Bestine Kazadi hivyo siwezi kuzungumza chochote kwa kuwa ni jambo ambalo bado halijatokea.”

Yanga kwa sasa wanahusishwa kwa karibu na usajili wa kiungo wa kati kutokana na Feisal ambaye hucheza kwenye eneo la kiungo kuomba kuondoka ndani ya timu hiyo, ukiachana na Feisal pia Yanga wanahusishwa na kumtaka kiungo Bobosi Byrahunga.

SOMA NA HII  MASHABIKI WA SIMBA V TP MAZEMBE WAPEWA TIKETI BURE NA SPOTI XTRA