Home Habari za michezo CHAMA ALAMBA DILI LA KIBABE

CHAMA ALAMBA DILI LA KIBABE

Habari za SImba SC

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama amesaini mkataba mpya wa binafsi na duka la vifaa vya michezo.

Chama amewaambia wafuasi wake kupitia Instagram kuwa anayo furaha kusaini mkataba huo.

“Nina furaha kuwajulisha kwamba nimesaini mkataba na @roby_sportswear ukiwa ni muendelezo wa ushirikiano wetu ambao tuliuanza miezi kadhaa iliyopita. Viatu vimekuwa ni sehemu muhimu kwenye utambulisho wangu, lakini pia kwa kila binadamu. Kwahiyo ushirikiano huu ni zaidi ya mimi kutangaza viatu tu, bali nitakuwa nafanya kitu ninachokipenda nje ya mpira.

Robby, endelea kutupendezesha ndugu yangu, sikukuu inakuja.”

SOMA NA HII  KOCHA WA SIMBA AFUNGUKA KILA KITU KUHUSU HALI YA KIKOSI CHA SIMBA