Home Habari za michezo DILI LA SIMBA SC LASHINDWA KUTIMIA…WAMEKOSA LAKINI WAMEPATA PIA….

DILI LA SIMBA SC LASHINDWA KUTIMIA…WAMEKOSA LAKINI WAMEPATA PIA….

Simba SC

KWENYE msako wa pointi 9 kanda ya Ziwa kikosi cha Simba SC kimegotea kwenye pointi 7 baada ya kuyeyusha pointi mbili.

Furushi la pointi 7 wanarejea nazo Dar wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi zao ni 41 vinara ni Yanga wenye pointi 47 wote wamecheza mechi 18.

Ni mechi tatu Simba SC chini ya Kocha Mkuu, Juma Mgunda imecheza ugenini ambapo ilikuwa Uwanja wa Kirumba, Geita Gold 0-5 Simba, Kagera Sugar 1-1 Simba Uwanja wa Kaitaba.

Ule mchezo wa tatu ulikuwa Uwanja wa Kirumba ubao ulisoma KMC 1-3 Simba SC.

Safu ya ulinzi ya Simba  imeokota nyavuni mabao mawili huku ile ya ushambuliaji ikitupia mabao 11.

Ni beki Henock Inonga yeye katupia kwenye mechi mbili mfululizo kanda ya Ziwa, aliwatungua Kagera Sugar na KMC.

SOMA NA HII  MASHABIKI SIMBA WACHANGANA KUNUNUA BASI JIPYA....