Home Habari za michezo MASHABIKI SIMBA WACHANGANA KUNUNUA BASI JIPYA….

MASHABIKI SIMBA WACHANGANA KUNUNUA BASI JIPYA….

Basi la Simba

Jumla ya kiasi cha Sh 42.4 milioni zimechangwa katika harambee maalumu ya kununua gari aina ya Coaster ambalo litasaidia mashabiki na wanachama wa Simba tawi la Mafinga wilayani ya Mufindi, mkoani Iringa kwa ajili ya safari zao kuisapoti timu yao pindi itakapokuwa ikicheza.

Hayo yamebainishwa leo Jumatatu, Desemab 19, 2022 na Mwenyekiti wa tawi la Simba Mafinga, Dickson Mtevele ( maarufu Villa) wakati akizungumza na wanahabari baada ya kumalizika kwa shughuli hiyo ambapo amesema wanawashukuru wanasimba kwa kujitokeza kwa wengi kwa ajili ya kufanikisha jambo hilo. Aidha Mwenyekiti huyo amesema kuwa katika harambee hiyo walilenga kukusanya kiasi cha Sh 62.9 milioni ambazo zinahitajika lakini hadi sasa wamefanikiwa kukusanya kiasi cha Sh42.4 milioni kwa ajili ya kukamilisha ununuzi wa basi hilo.

“Kama Mungu akitusaidia kufanikisha jambo letu ya ununuzi wa basi tutafurahi sana kwa sababu tayari tumeulizia gharama ya basi hilo kuwa ni Sh62.9 milioni lakini hadi sasa tumefikia asilimia 95 ya harambee yetu hivyo inatupa moyo kuwa jambo letu litafanikiwa,” amesema Mtevele

Pia Mtevele amesema kuwa kupatikana kwa basi hilo litakuwa msaada mkubwa kwao mbali na kutumiwa na mashabiki na wanachama kwa ajili ya kwenda kuisapoti timu yao lakini pia watalitimia kama chanzo cha kuwaingizia mapato katika tawi lao. Pia Mtevele amesema mbali na ununuzi wa basi hilo lakini mipango yao kama Tawi ni kuongeza idadi ya wanachama ambapo katika harambee wamepata zaidi ya Mashabiki na wanacha 500 wameweza kuhudhulia katika hafla hiyo.

Mtevele amesema kuwa wanasimba wameomba Mo dewji kuendelea kuisapoti Timu yao kuwa sehumu ambayo imebaki ili waweze kuendelea kwenda kushabikia Timu yao

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendego, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Saad Mtambule amesema kuwa baada ya kununuliwa kwa basi hilo hivyo kwa mara ya kwanza atasafiri na mashabiki na wanachama wa Tawi la Simba Mafinga kwa ajili kwenda Dar es Salaam kuishangilia Simba pindi itakapocheza katika uwanja wa Mkapa.

“Kwa mara ya kwanza nitaenda na nyinyi Dar es Salaam kwenda kushalingia timu yetu tena nitakaa siti ya nyuma baada ya kununua kwa basi hilo kwa siku hizi michezo ni ajira na uchumi tuendelee kushirikiana kwa pamoja tutaweza kufanikiwa kwa sababu umoja tulionao ni mkubwa,” amesema Mtambule

Kwa upande wake mwanachama wa simba kutoka Isalavanu tawi la Mafinga Charles Makoga amesema kuwa basi litakuwa na mchango mkubwa wa kukuza morali kwa wanasimba ikilinganishwa na kipindi cha nyuma ni mashabiki wa mjini pekee ambao walikuwa na uwezo wa kuchangia na kwenda kushangilia timu yao Nyanda za Juu Kusini kuishangilia.

“Mashabiki wa mjini ndio walikuwa wanaweza kwenda kuisapoti lakini kwa sasa baada ya kupatikana kwa basi hata wanachama na mashabiki wa pembezoni kama kata ya Isalavanu na ikongosi wataweza kwenda kuishangilia Timu yao,” amesema Makoga

Hata hivyo tawi la Simba Mafinga ndio tawi pekee litakuwa la kwanza hapa nchini kuwa na usafiri wao kwa ajili ya kwenda kuisapoti Timu yao Pindi itakapokuwa inacheza sehemu yoyote.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUFUNGA GOLI LA USHINDI JUZI....MUDATHIR KAIBUKA NA HILI JIPYA YANGA....