Home Habari za michezo WAKATI SIMBA WAKIMGWAYA….IHEFU NA GEITA ZAMMEZEA MATE KIBU DENIS…

WAKATI SIMBA WAKIMGWAYA….IHEFU NA GEITA ZAMMEZEA MATE KIBU DENIS…

Habari za Simba

Klabu ya Geita Gold imetuma ofa Simba ya kutaka saini ya mshambuliaji wake Kibu Denis kwa mkopo katika dirisha dogo la mwezi huu wa Desemba.

Gazeti la Mwanaspoti limethibitisha matajiri hao wa dhahabu wapo kwenye kusuka upya kikosi chao na pendekezo la kwanza kwenye eneo la ushambuliaji ni Kibu ambaye wanaamini atarithi mikoba ya George Mpole aliyetimkia FC Lupopo ya DR Congo.

Bado Simba na Kibu hawajajibu ombi hilo la Geita aliyoichezea kipindi ipo (Daraja la kwaza) kwa sasa Chamiponship kabla ya kujiunga na Mbeya City kisha Simba anayoitumikia kwa sasa.

Wakati huo huo taarifa kutoka Mbeya zinaeleza Ihefu nayo ipo kwenye hatua za mwisho za kutuma ofa Simba kumuomba Kibu kwa mkopo.

Kibu ndiye mfungaji bora wa msimu uliopita kwa Simba alipomaliza na mabao nane, na msimu huu hadi sasa ana bao moja alilolifunga juzi dhdi ya Geita wakati chama lake likiibuka na ushindi wa mabao 5-0.

SOMA NA HII  TUNZA TEREHE 30 YANGA WANAJAMBO LAO ZITO...VIFAA VIPYA KUANZA KUMIMINIKA KWA MFUMO WA LUKU...

1 COMMENT

  1. KUTOKA KUWA MKIMBIZI MPAKA KUSAJILIWA SIMBA SC….HAYA NDIO MAPITIO HALISI YA KIBU DENIS… - Bongo Soka

    […] mechi ya Simba kwa mara ya kwanza pale visiwani Zanzibar katika Kombe la Mapinduzi na kumtaja Kibu kama moja ya wachezaji alioridhishwa na ubora […]