Home Habari za michezo WAKATI AZAM WAKIENDELEA KUMUOTA FEI TOTO….BUMBULI AIBUKA NA KUWAUMBUA ….

WAKATI AZAM WAKIENDELEA KUMUOTA FEI TOTO….BUMBULI AIBUKA NA KUWAUMBUA ….

Habari za Yanga

Kufuatia Klabu ya Azam FC kutajwa kuwa mabosi wa timu hiyo wanaiwinda saini ya kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’, aliyewahi kuwa Ofisa Habari wa timu hiyo, Hassan Bumbuli amefichua kuwa hii sio mara ya kwanza Azam kumhitaji.

Tayari dirisha dogo la usajili Desemba 16, mwaka huu limefunguliwa timu mbalimbali zipo katika michakato ya kuboresha vikosi vyao kupitia usajili huku Azam wakitajwa kudhamiria kumng’oa Fei Toto Yanga.

Bumbuli alisema: “Dirisha la usajili limefunguliwa, hivyo ni wazi kutakuwa na vitu vingi vitazungumzwa kama ambavyo suala la Fei Toto lilivyojadiliwa katika siku za karibuni, lakini muda rasmi ukifika kila mmoja atafahamu.

“Mfano katika hili la Fei Toto siyo mara ya kwanza Azam kumhitaji, wakati mimi nikiwa Ofisa Habari wa Yanga waliwahi kuja kuulizia bei yake na tukawatajia lakini mpaka sasa Fei Toto yuko Yanga.”

Kuhusu usajili wa Fei Toto hivi karibuni Ofisa Habari wa muda wa Azam, Hasheem Ibwe alithibitisha kuwepo mpango huo kwa kusema, hakuna kitu ambacho kinashindikana na wakati ukifika kila kitu kitakuwa wazi na ukweli utajulikana.

SOMA NA HII  KUHUSU KLABU YA ULAYA KUMTAKA SAKHO KWA BIL 1.1 ZA KIBONGO...UKWELI WOTE HUU HAPA...