Home Habari za michezo BAADA YA KUMUONA MAYELE ANAVYOTETEMA TETEMA …TAMBWE KATIKISA KICHWA..KISHA AKASEMA HAYA..

BAADA YA KUMUONA MAYELE ANAVYOTETEMA TETEMA …TAMBWE KATIKISA KICHWA..KISHA AKASEMA HAYA..


STRAIKA wa zamani wa Simba, Mrundi, Amissi Tambwe, amemtaja Mkongomani, Fiston Mayele ndiye mshambuliaji bora ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu.

Tambwe ni kati ya washambuliaji waliokuwa tishio kipindi anacheza Ligi Kuu Bara akizitumikia Simba na Yanga ambapo huko kote aliwahi kuwa mfungaji bora.

Nyota huyo ni kati ya wachezaji waliofanikiwa kuipandisha DTB kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao ikitokea ChampionShip, wengine ni Tafadzwa Kutinyu, Nicholaus Gyan, James Kotei na Juma Abdul.

Tambwe alisema hakuna mjadala na ubishi, Mayele ni mshambuliaji bora msimu huu kutokana na kiwango kikubwa alinacho cha kufunga mabao.

Tambwe alisema licha ya ushindani wa ufungaji bora anaoupata kutoka kwa Geita Gold, George Mpole, lakini Mkongomani huyo ni bora zaidi.

“Msimu huu kwangu mshambuliaji bora ni Mayele anayeichezea Yanga, hilo amelithibitisha kutokana na kiwango bora cha kufunga mabao ambacho amekionesha.

“Ninaamini kama akiongeza bidii na wachezaji wenzake kumchezesha vizuri, basi atakuwa mfungaji bora.

“Nafahamu ushindani mkubwa upo wa ufungaji bora, lakini kutokana na ubora wa Yanga katika safu ya kiungo atafikia malengo ya kuchukua ufungaji bora,” alisema Tambwe.

Kabla ya mechi ya jana, Mayele alikuwa na mabao 12 sawa na Mpole, wote wakiwa vinara.

SOMA NA HII  MAYELE NA FEI TOTO WALIVYOPISHANA NA GARI LA MSHAHARA YANGA...