Home Habari za michezo BEKI WA WYDAD AMUIGA MAYELE…LIGI YA MABINGWA AFRIKA…ISHU NZIMA IKO HIVI

BEKI WA WYDAD AMUIGA MAYELE…LIGI YA MABINGWA AFRIKA…ISHU NZIMA IKO HIVI

BEKI WA WYDAD AMUIGA MAYELE...LIGI YA MABINGWA AFRIKA...ISHU NZIMA IKO HIVI

Baada ya mchezo wa juzi dhidi ya Simba Sc, Beki wa Wydad AC, raia wa Congo Arsene Zola amefunguka baada ya kuonekana akishangilia kwa staili ya “Kutetema” kama Mayele Fiston baada ya timu yake kupata bao la kwanza kupitia kwa Sambou Bouly.

Arsene alisema kuwa anafahamu ushindani uliopo kati ya Simba Sc na Yanga kupitia kwa wachezaji wenzake ambao pia ni raia wa Congo ndio sababu ya Kushangilia kwa style ya Mshambuliaji wa Yanga raia wa Congo Fiston Mayele.

Wydad ilishinda katika mchezo huo kwa bao 1-0 lakini katika matokeo ya jumla ilikuwa bao 1-1 hali iliyopelekea tinu hizo kwenda kwenye changamoto ya mikwaju ya penati ambapo Simba waliondolewa kwa kufungwa penati 4-3, na kuifanya Wydad kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mabingwa Afrika.

SOMA NA HII  ROBERTINHO ATANGAZA VITA KABLA YA MAMBO KUANZA, HAO POWER DYNAMO WAJIPANGE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here