Home Habari za michezo WAKATI ISHU YA INONGA IKIWA JUU JUU…COASTAL WAIKUNJULIA SIMBA KWA LAMECK LAWI…..

WAKATI ISHU YA INONGA IKIWA JUU JUU…COASTAL WAIKUNJULIA SIMBA KWA LAMECK LAWI…..

Habari za Simba leo

UONGOZI wa Coastal Union umeweka wazi juu ya kupokea ofa kutoka Simba ikihitaji huduma ya beki wao Lameck Lawi na ofa ya nyota huyo ni Million 200 za kitanzania.

Lawi amebakiza mkataba wa miaka miwili kutumikia Coastal Union na kuna taarifa kuwa Azam FC wameanza kumuwinda nyota huyo kupata huduma yake kwa msimu ujao wa Mashindano.

Ofisa habari wa Coastal Union, Abass Elsabri amethibitisha kupokea ofa kutoka Simba na kupewa thamani ya kumpata mchezaji huyo ni kiasi cha mill 200 za kitanzania.

Amesema suala la Azam FC ni tetesi bado hawajafika kwenye meza ya Coastal Union, sasa Simba wameonyesha nia na kuendelea na mazungumzo pande zote akiwemo mchezaji husika.

“Mkataba wa Lawi umebaki miaka miwili, Simba wamekuja na tuko nao mezani kutaka kununua mkataba huo mambo yakienda vizuri nadhani mchezji huyo atakuwa sehemu ya kikosi cha Simba msimu ujao.

Hatuna pingamizi suala la kuuza mchezaji, kama tuliweza kuwauza Abdi (Banda ), Mwamnyeto (Bakari) kipjndi cha nyuma iweje Lawi, tunafahamu soka ni biashara na kazi tutamuacha vijana wakatafute changamoto zingine,” amesema Abass.

Ameongeza kuwa milango ipo wazi kwa klabu zingine zinazohitaji na kuvutiwa na wachezaji wao ambao wanahitajika kuwasajili kwa kufuata taratibu zilizowekwa na mamlaka ya soka.

SOMA NA HII  KAHATA AWAAGA SIMBA SC AKIFICHUA SIRI KIBAO ZA GOMES..