Home Habari za michezo SIMBA WATAMBA, AL AHLY AMEKUJA KIPINDI KIBAYA

SIMBA WATAMBA, AL AHLY AMEKUJA KIPINDI KIBAYA

Habari za Simba leo

Klabu ya Simba imesema kuwa wapinzani wao kwenye michuano ya African Footbal League (AFL), Al Ahly wamekuja katika kipindi kibaya kwani Mnyama atawatafuna mapema mno.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally wakati akizungumza na wakazi wa Vingunguti kuelekea mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo kati ya Simba na Ahly utakaopigwa Ijumaa ijayo, Oktoba 20, 2023 katika Dimba la Mkapa.

“Ni hadhi kubwa tumepewa, ni heshima kubwa tumepewa wa kuwa mwenyeji wa mashindano haya AFL. AFCON mmeona imepatikana kwa nguvu kubwa baada ya mataifa matatu kuomba ndio tumepata lakini wenyeji wa AFL hatujaomba, wao wenyewe wameona tunastahili hatutakiwi kuchezea hiyo bahati.

“Tunataka watu wa AFL wakifika uwanjani siku hiyo waseme hawakukosea kuipa Simba wenyeji wa michuano hiyo. Lakini ili hili litimie lazima Wanasimba tukajaze uwanja, sio hilo tu lakini pia tuna kazi ya kumtoa Al Ahly mashindanoni.

“Tunawaheshimu Al Ahly lakini lazima watambue sisi ni Simba Sports Club, hakuna kinachoshindikana. Pira letu ni lilelile Pira Kokoto na sasa tunaongeza lingine Pira Machinjio.

“Sasa tumejipata lazima Al Ahly wajue hawaji kucheza na Simba changa, tumekomaa. Kila Mwanasimba aje uwanjani na tukifika ni sherehe mwanzo mwisho. Siku hiyo nenda kazini saa 5 asubuhi muage boss uwahi uwanjani,” amesema Ahmed Ally.

SOMA NA HII  GAMONDI PRESHA TUPU, BAADA YA WABONGO KUMGEUZIA KIBAO YANGA