Home Habari za michezo MRITHI WA MAYELE YANGA HALI TETE AKOSA PAKUSHIKA

MRITHI WA MAYELE YANGA HALI TETE AKOSA PAKUSHIKA

Mshambuliaji Emmanuel Mahop, aliyekuwa akihusishwa kujiunga na Yanga kwenye dirisha lililopita la usajili amerudi nchini Cameroon baada ya kufeli majaribio katika Klabu inayoshiriki Ligi daraja la kwanza nchini Saudi Arabia.

Mahop bado anahitajika na Canon Yaoundé ya nchini Cameroon ambapo kwenye klabu hiyo alifunga magoli kumi na nne (14) msimu uliopita lakini pia Dynamo Douala na Yanga wanawania kuipata saini yake dirisha lijalo la usajili.

Emmanuel Mahop ambaye ndiye alitajwa kuja kumrithi Fiston Mayele ndani ya Yanga, hana klabu anayoitumikia sasa baada ya kutoka nchini Saudi Arabia ila anakaribia kurejea Canon Yaoundé ili kuitumikia klabu hiyo.

Hata hivyo Yanga walimsajili Hafiz Konkoni kutoka Ghana ambaye na yeye hajaonyesha kiwango bora kama ambavyo Wananchi walitarajia.

SOMA NA HII  SAMATTA APATA DILI JINGINE, VILLA WAKISHUKA TU ANAIBUKIA HUKU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here