Home Habari za michezo KISA POLISI….YANGA WAMFICHA MAYELE NA FEI TOTO….ISHU NZIMA IKO HIVI….

KISA POLISI….YANGA WAMFICHA MAYELE NA FEI TOTO….ISHU NZIMA IKO HIVI….

Habari za Yanga

Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze amefunguka sababu za kuwaweka nje mastaa wake akiwemo Feisal Salum ‘Fei Toto’ katika mchezo wa kutinga hatua ya 32 bora ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), kuwa ni kuwaweka fiti kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Jumamosi dhidi ya Polisi Tanzania.

Yanga juzi walimenyana na Kurugenzi na kuikandamiza mabao 8-0, huku mshambuliaji Clement Mzize akiibuka shujaa kwa kutupia mabao manne kambani.

Akizungumza Kaze aliwapongeza mastaa wake kuiwezesha timu hiyo kutinga hatua inayofuata huku akitaja sababu ya kuwakosa Fiston Mayele na Fei Toto kuwa ni kuwapa nafasi ya kupumzika ili kujiandaa na mchezo wa ligi.

“Tunatarajia kucheza na Polisi Tanzania Jumamosi. Ni mchezo ambao utakuwa mgumu kwetu kutokana na kukutana na timu ambayo inatumia nguvu zaidi, hivyo wachezaji wanatakiwa kuwa na ubora ili kuonyesha ushindani. Mara nyingi timu za majeshi huwa ngumu sana lazima tuchukue tahadhari zote,” alisema na kuongeza:

“Yanga imesajili wachezaji ili wacheze hivyo kupata nafasi kwa wachezaji ambao wametumikia timu kwa dakika 90 na kuipa matokeo ni faida ya usajili mkubwa na tuna imani na kila mchezaji ndani ya timu.”

Kaze alisema wanatarajia mchezo mgumu na wa ushindani kutoka kwa Polisi na kukiri kuwa kuwapumzisha baadhi ya wachezaji kutawasaidia kupata matokeo mazuri ili waweze kuendeleza ushindani katika Ligi Kuu.

Alisema wanawaheshimu wapinzani wao na wanatambua ubora wao na ndio maana wamelichukulia kipaumbele suala hilo kwa kuwapa muda mastaa hao ili waweze kukabiliana na ushindani kutokana na kutambua ugumu kila wanapokutana na timu hiyo.

MZIZE NI BORA ASIFANANISHWE NA MAYELE

Wakati huohuo Kaze alimzungumzia Mzize kuwa ni mchezaji mzuri ambaye anafundishika na ni mwepesi kuelewa, lakini bado anahitaji nafasi zaidi ili kufikia kiwango bora ambacho kitamfanya awe mchezaji tishio.

“Ni kweli ni mchezaji mzuri na muhimu ndani ya timu, lakini anahitaji kuendelea kujifunza zaidi ili kufikia ubora unaotakiwa sio mchezaji ambaye anafaa kufananishwa na Mayele kwa sasa ni mapema sana,” alisema.

“Tunatambua mchango wake na ndio maana tumekuwa tukimpa nafasi ya kucheza na ataendelea kuipata kutokana na timu kumuhitaji na namna ratiba ilivyo sasa.”

SOMA NA HII  'KAZI CHAFU' ZA CHE MALONE NA KENNEDY JUMA ZAMFANYA MBRZAILI SIMBA KUFUNGUKA HILI...