Home Habari za michezo ‘KAZI CHAFU’ ZA CHE MALONE NA KENNEDY JUMA ZAMFANYA MBRZAILI SIMBA KUFUNGUKA...

‘KAZI CHAFU’ ZA CHE MALONE NA KENNEDY JUMA ZAMFANYA MBRZAILI SIMBA KUFUNGUKA HILI…

Habari za Simba

Kocha wa Simba SC, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema baada ya timu yake kuwa na uwezo wa kufunga kila mechi, lakini bado kuna tatizo la mawasiliano katika safu ya ulinzi licha ya Che Malone Fondoh na Kennedy Juma kucheza vizuri. Simba imecheza mechi tano za ligi mpaka sasa, lakini ikiruhusu mabao matatu. .

Robertinho amewapongeza wachezaji wake kupata matokeo mazuri na kuiweka timu hiyo kileleni mwa msimamo wa ligi, lakini hafurahii kuendelea kuruhusu mabao licha ya ushindi. Kocha huyo amebaini tatizo katika safu ya ulinzi akisema bado haichezi kwa muunganiko mzuri ikiwa na makosa rahisi ya kujisahau.

“Kwa muda mrefu tumekuwa tunamtumia Inonga (Henock), lakini sasa hayupo tunawatumia Che Malone na Kennedy. Wanafanya kazi kubwa, lakini tunatakiwa kuwaongezea kitu,” alisema kocha huyo.

“Tunaweza kufunga mabao, lakini tunatakiwa kuongeza umakini na kuimarisha mawasiliano mazuri na mabeki wetu, ili wasiruhusu mabao katika mechi zijazo kwani zitakuwa ni mechi ngumu.”

Robertinho alisema watatumia muda wa mapumziko wa kalenda ya kimataifa kuwaongezea ubora mabeki kabla ya kurudi kwenye mechi zijazo. Hizi siku nitakaa nao ili kuondoa makosa niliyoyaona katika michezo hii ya ligi kwani sikuweza kuwabadilisha kutokana na ratiba ngumu ya mfululizo wa mechi zilizokuwepo. Naamini bado tunaweza kufanya vizuri kabla ya mechi ya Super League dhidi ya Al Ahly na Ligi ya Mabingwa Afrika,” amesema Robertinho.

SOMA NA HII  KUELEKEA SIMBA DAY: MZEE DALALI AFUNGUKA HAYA..WADAU WAIJIA JUU SIMBA..WATAKA APEWE NYUMBA