Home Habari za michezo MKANDA MZIMA WA SAKATA LA MWAKINYO HUU HAPA….ISHU YA KUMGOMBEA DEMU YATAJWA…

MKANDA MZIMA WA SAKATA LA MWAKINYO HUU HAPA….ISHU YA KUMGOMBEA DEMU YATAJWA…

Habari za Michezo

Hisia za Mwakinyo na msimamo wa promota, ndivyo vitu ambavyo viko nyuma ya pazia katika sakata la bondia huyo nyota nchini kugoma kupanda ulingoni Septemba 29.

Mwakinyo aligomea pambano hilo, siku moja kabla na kuondoka kurejea kwao, Tanga akitokea Dar es Salaam huku promota akifunguka sababu kadha wa kadha zilizopelekea bondia huyo kugoma.

Miongoni mwa vitu vilivyotajwa na kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari ni bondia huyo namba moja kwenye uzani wa super welter ni kumkataa kila bondia aliyeletewa kupigana naye.

Awali, Mwakinyo alisaini kuzichapa na Okwiri, kabla ya kubadilushiwa mpinzani dakika za mwishoni na kuletewa Julius Indongo.

Sababu nyingine iliyotajwa ni kutaka cha juu kwa bondia ambaye yeye Mwakinyo ndiye alimchagua wazichape naye, pia kumkataa mmoja wa wadhamini wa pambano hilo na jambo jingine ni kuwepo ugomvi wa mwanamke.

Nyuma ya pazia ni hivi

Katika mahojiano na Mwananchi, Mwakinyo anafunguka ishu yote huku mtu wa karibu wa bondia huyo akiweka wazi chanzo cha yote hayo ni hisia za bondia huyo na msimamo wa promota.

“Kwa makubaliano ya mdomo, Mwakinyo yuko sahihi, lakini kimaandishi, promota yuko sahihi, walikubaliana vingine yeye akaenda kinyume.

“Kwenye ishu ya mdhamini, sio kama Mwakinyo alichagua, isipokuwa mmoja kati yao amesababisha mtafaruku wa bondia huyo na kaka yake.

“Mwakinyo hazungumzi na kaka yake sababu ya huyo mtu, Mwakinyo anaona ni kama amemharibia maisha yake, aliona kupanda ulingoni akitumia brand (chapa) ya huyo mtu ni kama udhalilishaji dhidi yake, hakuwa na shida na wadhamini, isipokuwa huyo mmoja wana ugomvi wa kifamilia,” anasema.

Anasema chanzo cha ugomvi wao kilianza kwenye pambano la Mwakinyo na Tinampay, miaka kadhaa iliyopita.

“Huyo (anamtaja promota Mwakinyo aliyemkataa) alishiriki kutafuta pesa kwa ajili ya mashabiki kwenda Dar es Salaam kumsapoti Mwakinyo dhidi ya Tinampay.

“Aliposikia alikasirika, mashabiki nao wakamkasirikia ni kwanini achukue (anamtaja yule mdhamini Mwakinyo aliyemkataa) kufanya kitu kizuri, hata hivyo zoezi hilo liliendelea, ilipatikana milioni akapewa Mwakinyo, kuanzia pale hakukuwa na maelewano baina yao.

Mtu huyo wa karibu wa Mwakinyo anasema kuna baadhi ya mabondia ambao walikuwa kambi moja walikosana sababu ya ukaribu wao na huyo mdhamini, ugomvi wao ni wa muda mrefu,”.

Huyu hapa Mwakinyo

Mwakinyo ametema nyongo, akifunguka kuhusu madai yote ambayo yalielekezwa kwake na kutajwa kuwa chanzo cha mgomo huo akianza na ishu ya kumkataa kila bondia

“Sio kweli, kilichotokea bajeti yao ilikuwa dola 5000, bondia alitaka dola 15,000 akashuka hadi 10,000, ikafikia hatua wakataka waniletee mabondia ambao hawakidhi vigezo, wa renki ya chini mno, hata mabadiliko kutoka kucheza na Okwiri hadi Indongo ni kushindwana kwenye maslahi.

Kutaka cha juu

Mwakinyo anasema, hajawahi kufanya kitu hicho, akidai bajeti ya kumlipa mpinzani wake ilikuwa ni dola 5000.

“Kama ningekuwa nataka cha juu ningekubali dola 3000 ya kuongezea kwa Indongo tutoe sisi?,” alihoji Mwakinyo na kuendelea.

“Indongo yeye alitaka dola 10,000, akashuka hadi dola 8000, promota akasema bajeti yake ni dola 5000 tu, haiongezeki zaidi ya hapo tukakubaliana dola 3000 tutatoa sisi, sasa kuongeza cha juu kunatokea wapi?.

“Kwanza mkataba wa pambano langu na Okwiri uliharibika, promota akinionyesha mkataba, sikusaini mkataba kucheza na Indongo,” anasema.

Ingawa rais wa Kamisheni ya Ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC), Chaurembo Palasa anasema bondia anapobadilishiwa mpinzani, mkataba unabaki ule ule wa awali.

“Anatakiwa kupewa taarifa saa 72 kabla ya pambano na promota, huo ndio utaratibu, ingawa mkataba utabaki ule ule,” anasema Palasa.

Ugomvi wa mwanamke

Kingine ambacho kilitajwa kuwa chanzo cha bondia huyo kugomea pambano ni kugombea mwanamke, jambo ambalo Mwakinyo anadai halina ukweli.

“Promota alitoka nje ya makubaliano, basi hayo mengine ni maneno tu yatazungumzwa sababu yametokea yaliyotokea.

SOMA NA HII  SIKU CHACHE BAADA YA KUITWA TENA TAIFA STARS...ABDI BANDA AWARUSHIA MASTAA WENZAKE UJUMBE HUU 'LIVE'...