Home Uncategorized MESSI: TULICHELEWA KUKATWA MSHAHARA

MESSI: TULICHELEWA KUKATWA MSHAHARA

LIONEL Messi nahodha wa Barcelona, amesema kuwa jambo la wachezaji kukatwa mshahara limechelewa kufanyika kwa sababu wachezaji walikuwa wanapambana kuisadia klabu pamoja na kuwasiaidia wale walioathirika.

Hatua hiyo ya kukatwa mshahara huo ni kwa ajili ya kuwachangia wafanyakazi wa Barcelona kulipwa mshahara pamoja nakuwasaidia waathirika wa Virusi vya Corona.

Uongozi wa Barcelona umekubaliana kuwakata wachezaji  asilimia 70 ya mishahara.

Messi,amesema:- “Kwetu wakati umefika, tutakatwa asilimia 70 ya mishahara yetu katika kipindi hiki. Pia tutaisaidia klabu ili wafanyakazi wengine walipwe asilimia 100 ya mishahara yao nadhani suala hili lilichelewa,” .

SOMA NA HII  WANA MICHEZO WANA NGUVU KUBWA KULIKO HATA WANASIASA IWAPO WATAFANYA HIVI