Home Habari za michezo USHINDI WA KISHINDO WA SIMBA JANA WAIIBUA SERIKALI…WAZIRI ATOA AIGIZO ‘LA LAZIMA’…

USHINDI WA KISHINDO WA SIMBA JANA WAIIBUA SERIKALI…WAZIRI ATOA AIGIZO ‘LA LAZIMA’…


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ameipongeza  timu ya Simba kwa kufuzu kuingia robo fainali ya ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika baada ya kuibamiza vibaya timu ya US Gendarmerie 4-0 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mhe. Mchengerwa ametoa pongezi hizo, baada ya kumalizika kwa mpambano huo ambapo amesema ushindi huo ni ushindi wa kihistoria.

“Ninaipongeza timu ya Simba kwa ushindi wa kishindo kuelekea kwenye robo fainali ya mashindano ya shirikisho la mpira wa miguu la Afrika. kama taifa, tunajivunia kwa ushindi huo mnono unaoitangaza nchi yetu kimataifa.” amesema  Waziri  Mchengerwa.

Vilevile waziri Mchengerwa ameitaka timu ya Simba kufanya maandalizi ya kutosha ili kuweza kufanya vizuri zaidi katika mashindano hayo hatimaye kuchukua kombe na kuendelea kuitangaza Tanzania duniani.

Simba kwenye michuano ya robo fainali inaweza kukutana na TP Mazembe(DR Congo), Orlando Pirates ( Afrika Kusini) na Al Ahly Tripoli (Libya).

Ukiachilia timu hizi nne(4) timu nyingine nne(4) ambazo zimefuzu kuingia robo fainali ya mashindano haya ni pamoja na RS Berkane (Morocco), Pyramids (Misri), Al-Ittihad (Libya) na Al Masry Misri.

Simba inatarajiwa kuanzia nyumbani Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  KIGOGO WA SOKA AFRIKA AVUNJA UKIMYA..."YANGA INA NGUVU KUBWA SANA