Home Habari za michezo BAADA YA KUPOKEA KICHAPO CHA ‘HAJA’ JANA…KOCHA USGN KAONA ISIWE TABU…KAFUNGUKA HAYA...

BAADA YA KUPOKEA KICHAPO CHA ‘HAJA’ JANA…KOCHA USGN KAONA ISIWE TABU…KAFUNGUKA HAYA ….


Kocha Mkuu wa USGN Zakariou Ibrahimu amesema uchanga wa kikosi chake, umefanya wapoteze mchezo wa mwisho wa ‘Kundi D’ Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Simba SC ya Tanzania.

USGN ilipoteza kwa 4-0 jana Jumapili (April 03), Uwanja wa Benjamin Mkapa na kutupwa nje ya Michuano ya Kombe la Shirikisho msimu huu 2021/22.

Kocha Zakariou amesema Wachezaji wake wengi hawana uzoefu wa kutosha kwenye michuano ya Kimataifa, kwani miongoni mwao wanashiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo.

Hata hivyo Kocha huyo kutoka nchini Niger amewapongeza wachezaji wake kwa kuonyesha soka safi kipindi cha kwanza na kufanikiwa kuibana Simba SC, licha ya mambo kuwaendelea kombo kipindi cha pili ambapo waliruhusu kufungwa mabao 4-0.

Tulikuwa bora kipindi cha kwanza lakini kipindi cha pili tulifanya makosa mengi, Timu yetu bado changa tutaendelea kupambana ili tuwe bora siku za usoni, baadhi ya wachezaji wangu ndo mara yao ya kwanza kushiriki Michuano hii”

Katika hatua nyingine Kocha Zakariou, amewapongeza Simba SC kwa kufanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali, na amewatakia kila la kheri katika hatua hiyo ili waweze kupita na kusonga mbele zaidi.

“Niwapongeza Simba SC kwa kucheza vizuri dhidi ya kikosi changu, wameonyesha uzefu wao katika michuano hii mikubwa Barani Afrika, niwatakie kila la kheri katika hatua ya Robo Fainali na itapendeza kuwaona wakifika mbali zaidi.” amesema Kocha Zakariou Ibrahim

Simba SC imemaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Kundi D, ikifikisha alama 10 sawa na RS Berkane ya Morocco inayoongoza kundi hilo kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

ASEC Mimosas ya Ivory Coast imemaliza katika nafasi ya tatu ikiwa na alama 09 huku USGN ikiendelea kuburuza mkia kwa kuwa na alama 05.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA HAOMBI MSAMAHA WALA HANA SHIDA...SIMBA WAMCHIMBWA MKWARA WA KUFA MTU MORRISON...