Home Habari za michezo NDOA YA SIMBA NA ONYANGO YAZIDI KUPIGWA WIMBI…GOR MAHIA WAIBUKA KUMUOKOA…

NDOA YA SIMBA NA ONYANGO YAZIDI KUPIGWA WIMBI…GOR MAHIA WAIBUKA KUMUOKOA…

Tetesi za Usajili Simba

KLABU ya Gor Mahia ya nchini Kenya imeanza mazungumzo na beki wa Simba, Joash Onyango kwa ajili ya msimu ujao.

Beki huyo raia wa Kenya licha ya kucheza mara kwa mara ndani ya kikosi hicho, huenda akarejea kwao baada ya msimu huu kuisha kutokana na kile kinachoonekana kutokubalika na mashabiki wengi.

Mbali na hilo,pia inatajwa kuwa beki huyo hana mahusiano mazuri na wachezaji wenzake kutokana na kuwa mtu wa misimamo kupitiliza.

Onyango ambaye alitua Simba misimu mitatu iliyopita akiwa kama mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Kenya, ameshuhudiwa akiwa kwenye kiwango cha kupanda na kushuka japo kuwa amefanikiwa kuwa na uhakika wa namba kwenyeΒ  kikosi cha kwanza.

Mashabiki wengi wa soka nchini, wamekuwa wakimtania kutokana na kuwa na muonekano wa ‘kifaza’ zaidi huku yeye mweyewe akisema ana miaka chini ya 30.

Katika misimu aliyocheza soka na Simba, Onyango amefanikiwa kucheza robo fainal tatu za CAF, ambazo mbili ni za Ligi ya mabingwa na moja ni ya kombe la shirikisho, huku pia akishindwa mara tatu ubingwa wa ligi kuu.

Hata hivyo licha ya Gor Mahia kumhitaji, Singida Big Stars nayo inahitaji saini yake ili kwenda kuimarisha kikosi chao ambacho msimu ujao pasi na shaka watashiriki mashindan ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Endapo atatua Singida Big Stars, Nyota huyo pia wa timu ya taifa ya Kenya, atakuwa anaungan na wachezaji wenzake wa zamani waliotamba na Simba kama Medie Kagere,Pascal Wawa pamoja na Said Ndemla bila kumsahahu Ibrahim Ajib.

SOMA NA HII  WAZUNGU WAJITOSA KUIOKOA GEITA GOLD...ISHU NZIMA IKO HIVI....