Home Habari za michezo KAMBI YA SIMBA DUBAI YAJIBU….AHMED ALLY AFUNGUKA WALICHOPEWA NA CSKA MOSCOW…

KAMBI YA SIMBA DUBAI YAJIBU….AHMED ALLY AFUNGUKA WALICHOPEWA NA CSKA MOSCOW…

Habari za Simba

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema kambi ya siku ya nane waliofanya Mjini Dubai imewapa mafanikio kwa kuwa Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amepata muda wa kukaa pamoja na wachezaji.

Ahmed amesema baada ya Robertinho kukaa na wachezaji amewasoma tabia zao za ndani na nje ya uwanja hivyo itakuwa faida kwake kuwaongoza katika mechi za mashindano.

Itakumbukwa kuwa Simba mbali na ligi kuu, pia inatarajiwa kushiriki hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa afrika mwezi ujao.

“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumerejea salama jijini Dar es Salaam na kesho tutashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Mbeya City kwenye Ligi Kuu ya NBC.”

“Kambi yetu ilikuwa ya mafanikio mjini Dubai Kocha Robertinho amepata nafasi ya kukaa na wachezaji pia tumepata mechi nzuri za kirafiki ambazo zimetuonyesha mahali kikosi chetu kilipo kuelekea michuano iliyo mbele yetu,” amesema Ahmed.

kwa upande mwingine Msemaji huyo amesema mechi mbili za kirafiki walizocheza zilikuwa kipimo kizuri kwao, kwa michuano ya ndani bali hadi Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo itaendelea mwezi ujao.

Simba kesho itajitupa uwanjani kuikaribisha Mbeya City katika muendelezo wa ratiba ya Ligi Kuu ya NBC.

SOMA NA HII  CHAMA NA AZIZ KI WALIVYOMALIZA MICHUANO YA CAF KIBABE...REKODI ZAO NI BALAA...