Home Habari za michezo HUSSEIN KAZI NA SIMBA NDIO BASI TENA….KUPISHANA NA LAMECK LAWI MLANGONI…

HUSSEIN KAZI NA SIMBA NDIO BASI TENA….KUPISHANA NA LAMECK LAWI MLANGONI…

Habari za Simba leo

Mlinzi wa kati wa klabu Simba Hussein Kazi inatajwa kuwa ni sehemu ya kukamilisha dili la Usajili la Mlinzi wa kati wa klabu ya Coastal Union Lameck Lawi,

Simba imetoa Kiasi cha pesa pamoja na Hussein kazi ili kukamilisha dili hilo ambalo lilikuwa la wengi kuelekea soko la usajili.

Haikuwa rahisi kwa klabu ya Coastal Union kutupilia mbali ofa za Vilabu vya Ihefu na Azam FC ambao nao walituma ofa ya kumtaka Lameck Lawi.

Hussein Kazi amesajiliwa na Simba mwanzoni mwa msimu huu, ambapo alitazamiwa kutoa ushindani kwa wachezaji wa kikosi cha kwanza kwenye  timu hiyo hali ambayo ni kama imeshindikanika.

Simba wanatazamia kufanya maboresho makubwa ya kikosi chao kuelekea msimu ujao haswa mara baada ya kufanya vibaya msimu huu.

Inataarifiwa kuwa moja ya maeneo ambayo Simba wanaweza kufanya vyema ni pamoja na Usajili wa Beki, kiungo na mshambulaiji huku eneo la ufundi wakitazamia kuleta kocha mwenye rekodi kubwa kuja kufanya kazi na Mgunda.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE