Home news WAKATI TIMU IKO ZNZ…’VIFAA VIPYA ‘YANGA NI FULL JEURI….UONGOZI WASHINDWA KUJIZUIA…WAANIKA HAYA..

WAKATI TIMU IKO ZNZ…’VIFAA VIPYA ‘YANGA NI FULL JEURI….UONGOZI WASHINDWA KUJIZUIA…WAANIKA HAYA..


NYOTA wapya wa timu ya Yanga ambao wametua ndani ya dirisha dogo, wameipa jeuri timu hiyo kiasi cha kutamka kuwa wana uhakika wa kutetea ubingwa wao wa Kombe la Mapinduzi.

Mabosi hao wameongeza kuwa wana uhakika huo kwa mastaa hao wapya ndani ya kikosi hicho, wakiamini wana uwezo mkubwa.

Miongoni mwa mastaa wapya ambao wamesajiliwa na Yanga ni Dennis Nkane aliyetoka Biashara United, Aboutwalib Mshery, Salim Aboubakhari ‘Sure Boy’ na Crispin Ngushi.

Yanga ni mabingwa watetezi na juzi walitoka sare  dhidi ya KMKM katika mchezo wa pili wa Mapinduzi, baada ya ule wa kwanza kupata ushindi mbele ya Taifa Jang’ombe kushinda kwa mabao 2-0.

Mkuu wa Kitengo cha Habari Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa wachezaji walionao ni wazuri, jambo ambalo linawapa imani ya kuweza kutwaa taji la Mapinduzi.

“Sisi ni mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi na tunaweka wazi kwamba dhamira yetu ipo wazi kwamba tunahitaji kulitwaa taji hili na inawezekana hasa ukizingatia kila mchezaji ana uwezo mkubwa na anahitaji kufanya jambo.

“Uwepo wao wa wachezaji wapya pamoja na wale wengine ambao wapo kwa muda inatosha kusema kwamba nini ambacho tunahitaji kukifanya, kilichobaki ni suala la kusubiri na kuona,” alisema Bumbuli.

SOMA NA HII  RUVU SHOOTING : TUTAIFUNGA NAMUNGO