Home news YANGA WAVUNJA UKIMYA KUHUSU SINTOFAHAMU YA AUCHO NA BANGALA…WATOA TAMKO HILI…

YANGA WAVUNJA UKIMYA KUHUSU SINTOFAHAMU YA AUCHO NA BANGALA…WATOA TAMKO HILI…


UONGOZI wa Yanga, umeweka wazi kuwa wachezaji wao Khalid Aucho, Yanick Bangala, Djuma Shabani na Mukoko Tonombe, watapatikana katika mchezo unaofuata wa nusu fainali ya Kombe la mapinduzi dhidi ya Azam FC.

Yanga imetinga hatua hiyo mara baada ya kumaliza vinara wa Kundi B kwa kukusanya pointi nne na kesho Jumatatu itacheza dhidi ya Azam FC.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, aliweka wazi kuwa: “Wachezaji wetu ambao walijiunga na timu ya taifa ya DR Congo, Yanick Bangala, Djuma Shabani na Mukoko Tonombe tayari wameshamaliza mechi yao ya timu ya taifa Januari 6, hivyo itawachukua siku mbili mpaka kufika huku Zanzibar.

“Aucho pia atapatikana katika mchezo unaofuata mara baada ya kumalizika kwa mapumziko yake nchini Uganda, hivyo wapenzi wa Yanga wasiwe na wasiwasi kwani malengo yetu ni yale yale kuhakikisha kuwa tunatwaa ubingwa huu.”

“Tumefanya mabadiliko kidogo ya kikosi kwa ajili ya kuwalinda wachezaji wetu na majeraha na kuwapa naafasi wengine wacheze ila haina maana hatutaki ubingwa. Wanasimba wawe na imani kuwa tutafanya vizuri.”

Kesho Jumatatu, Simba wanatarajiwa kucheza nusu fainali dhidi ya Namungo, kama watashinda watacheza fainali na mshindi kati ya Yanga na Azam FC.

SOMA NA HII  MANULA NA WACHEZAJI HAWA WENGINE KUUKOSA MCHEZO WA LEO...KOCHA BIASHARA 'ACHEKELEA KOONI'....